Mchezaji wa klabu Neal Maupay anakaribia kujiunga na klabu ya Everton akitokea klabu ya Brighton Hove Albion.

Mshambuliaji huyo raia wa Kifaransa ambae amekua na wakati mzuri katika klabu yake ya Brighton chini ya mwalimu Graham Potter akiunda safu ya ushambuliaji na wachezaji kama Trossard,pamoja na Dnny Welbeck.

maupay, Maupay Kujiunga Everton Hivi Karibuni., Meridianbet

Mchezaji huyo wa zamani wa vilabu vya Saint Etienne na Brest vya chini Ufaransa amepanga kujiunga na klabu ya Everton the Toffees  ambayo imeanza vibaya msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza chini ya mwalimu Frank Lampard.

klabu ya Everton inapambana kujiweka vizuri haswa katika eneo lao la ushambuliaji baada ya kuondokewa na mshambuliaji wao hatari raia wa Brazil Richarlison alietimkia kunako klabu ya Tottenham Hotspurs.

Wakati huhuo klabu ya Chelsea nayo inapambana kumchukua mshambuliaji kinda wa klabu hiyo raia wa Uingereza Anthony Gordon. Hali inafanya Everton kuingia sokoni nna kuimarisha kikosi haswa eneo lao la ushambuliaji na wameanza na Neal Maupay.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa