Kylian Mbappe amefurahia kufikisha mabao mia moja tangu aanze kuvaa jezi ya Paris Saint-Germain baada ya kufunga siku ya Jumamosi katika mchezo wa Ligue 1.

Mbappe alifikisha magoli 99 katika mashindano yote ya PSG wakati alipofunga mara mbili dhidi ya kilabu yake ya zamani ya Monaco kwa kichapo cha 3-2 Novemba 20.

Alishindwa kutikisa wavu katika mechi tatu – dhidi ya RB Leipzig, Bordeaux na Manchester United – kabla ya kuongeza idadi ya magoli kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Montpellier.

Huku Moise Kean akiwa ameifungia PSG bao la kuongoza katika dakika ya 77, Mbappe alikuja kupata bao kwa jaribio lake moja na kuipatia point timu ya Thomas Tuchel katika dakika za lala salama.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amepachika mabao 74 kati ya 100 aliyoifungia PSG katika ligi kuu ya Ufaransa, huku magoli 13 kwenye Ligi ya Mabingwa.

Mabao yake 13 yaliyosalia amefunga katika mashindano ya Ufaransa ya kombe la nyumbani na Trophee des Champions.

“Nilijua takwimu zangu, ndio. Ilikuwa mechi chache ambazo nilitaka kupata alama ya 100,” aliiambia Canal +.

“Asante kwa wachezaji wenzangu na kwa kilabu kwa kunipa ujasiri, iwe katika nyakati nzuri au mbaya. Asante kwa kila mtu anayefanya kazi huko.

Mbappe ni wa nne, pamoja na Dominique Rocheteau, katika orodha ya wafungaji bora wa PSG, nyuma ya Pauleta (109), Zlatan Ibrahimovic (156) na Edinson Cavani (200).

“Kufunga mabao 200 na PSG? Nani anajua,” alisema Mbappe, ambaye mara nyingi amekuwa akihusishwa kuhamia kwa miamba ya LaLiga Real Madrid na Barcelona. “Sikuwahi kufikiria magoli 100! Lazima ufikirie juu ya mchezo ujao.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Mbappe, Mbappe Afikisha Magoli 100 kwa PSG., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

24 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa