LICHA ya kupata bao la kuongoza mapema kupitia kwa mzawa Nickosn Kibabage ilikuwa ngumu kwa Mtiwa Sugar kusepa na pointi tatu za Mbeya City kwenye mechi ya jana Jumapili kwenye uwanja wa Manungu.

Bao la mapema kwa Mtibwa Sugar lilijazwa kimiani na na mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage dakika ya kwanza, bao la pili likafungwa na Jean Pipi dakika ya 29.

Uongozi wao ulikuwa kwa muda wa dakika 54 kwa kuwa kipindi cha pili mabao yote yaliwekwa usawa. Ilikuwa dakika ya 55 kwa shuti la Hassan Nassoro kugonga mwamba kumfanya kipa Faroukh Shikalo kwenye harakati za kuokoa mpira ukimgonga kwenye mgongo na kuzama nyavuni.

Bao la pili ni mali ya Tariq Seif dakika 65 na kufanya ubao uwe na usawa.
Sasa Mtibwa Sugar ni nafasi ya 7 pointi 8 na Mbeya City nafasi ya 10 pointi 5 zote zimecheza mechi tano.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa