Mbwana Samatta Astaafu Rasmi Taifa Stars Baada ya Miaka 15

Nahodha wa muda mrefu wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, ametangaza rasmi kustaafu kuichezea Taifa Stars, akihitimisha safari yake ya takribani miaka 15 akiwa sehemu ya kikosi hicho. Samatta amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutafakari kwa kina, huku akieleza kuwa amejivunia kuitumikia nchi yake katika kipindi chote alichokuwa mchezaji wa timu ya taifa.

Mbwana Samatta Astaafu Rasmi Taifa Stars Baada ya Miaka 15 Katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne, Julai 7, 2026, Samatta amesema safari yake na Taifa Stars imekuwa na mchanganyiko wa mafanikio, changamoto na kumbukumbu nyingi ambazo hazitasahaulika. Mshambuliaji huyo amebainisha kuwa moja ya mafanikio makubwa kwake ni kupewa nafasi ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka 10 akiwa nahodha.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Ninaamini huu ni wakati wa vizazi vipya kupewa nafasi ya kutufikisha kwenye hatua za juu zaidi,” amesema Samatta katika taarifa yake, akieleza imani yake kwa wachezaji chipukizi watakaokuja kuendeleza alipoishia.

Mbwana Samatta Astaafu Rasmi Taifa Stars Baada ya Miaka 15 Katika kipindi chake akiwa nahodha, Samatta alishuhudia Taifa Stars ikifuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mara tatu, pamoja na kuweka historia ya kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza. Mafanikio hayo yameifanya safari yake kuwa moja ya vipindi muhimu katika historia ya soka la Tanzania.

Mbwana Samatta Astaafu Rasmi Taifa Stars Baada ya Miaka 15 Samatta pia ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa mchango wao katika maendeleo ya soka nchini. Ameeleza kuwa ataendelea kuwa mshauri na mfuasi wa Taifa Stars huku akiamini timu hiyo itaendelea kufanya vizuri chini ya kizazi kipya cha wachezaji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.