McFarlane Awatetea Wachezaji wa Chelsea Baada ya Kichapo Kutoka kwa Nottingham Forest

Kocha wa muda wa Chelsea FC, Calum McFarlane, amewatetea wachezaji wake akisisitiza kuwa walionyesha kujituma licha ya kupokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Jumatatu kwenye dimba la Stamford Bridge. Matokeo hayo yamezidi kudhoofisha matumaini ya Chelsea kufuzu michuano ya UEFA Champions League msimu ujao.

McFarlane Awatetea Wachezaji wa Chelsea Baada ya Kichapo Kutoka kwa Nottingham ForestKatika mchezo huo, Taiwo Awoniyi aliifungia Forest bao la kwanza mapema kabla ya Igor Jesus kufunga la pili kwa mkwaju wa penalti. Hali ilizidi kuwa mbaya kwa Chelsea pale Cole Palmer alipokosa penalti mwishoni mwa kipindi cha kwanza, huku Awoniyi akiongeza bao la pili kwake kipindi cha pili. Bao la kuvutia la mkasi lililofungwa na Joao Pedro halikutosha kuipa nafuu Chelsea.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo, McFarlane alisema “Ilikuwa ni matokeo na kiwango cha kusikitisha. Dakika 15 za mwanzo hazikuwa nzuri kabisa, na hilo ndilo lililoathiri mchezo mzima.” Aliongeza kuwa bado anahitaji kuutazama upya mchezo huo ili kuelewa tofauti kubwa ya kiwango walichoonyesha ukilinganisha na mechi iliyopita dhidi ya Leeds United.

McFarlane Awatetea Wachezaji wa Chelsea Baada ya Kichapo Kutoka kwa Nottingham ForestMcFarlane pia aligusia nafasi walizokosa, akisema “Enzo Fernandez alipiga mpira ukagonga mwamba na Cole Palmer akakosa penalti. Unapoanza vibaya, unahitaji bahati katika matukio kama hayo lakini haikuwa upande wetu. Tunajua tuna uwezo mkubwa zaidi ya tulichoonyesha.”

McFarlane Awatetea Wachezaji wa Chelsea Baada ya Kichapo Kutoka kwa Nottingham ForestLicha ya tetesi zilizokuwepo kuhusu kukosekana kwa ari kwa wachezaji wakati wa kocha wa zamani Liam Rosenior, McFarlane alisisitiza: “Sidhani kama kulikuwa na ukosefu wa juhudi au kujituma. Tunawaona wachezaji kila siku na wanajitahidi kwa kila namna. Tunahitaji kuboresha kiwango na kujipanga kwa mchezo ujao.”

McFarlane Awatetea Wachezaji wa Chelsea Baada ya Kichapo Kutoka kwa Nottingham ForestMbali na matokeo hayo mabaya, Chelsea pia ilipata pigo baada ya kinda Jesse Derry kuumia kichwani katika mechi yake ya kwanza na kutolewa nje kwa machela. McFarlane alitoa taarifa ya hali yake akisema “Yuko katika hali nzuri kwa sasa. Nitazungumza zaidi na madaktari, lakini dalili zinaonesha hali ni ya kuridhisha.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.