Wakala maarufu wa soka, Jorge Mendes, ameweka wazi hatma ya nyota wa Paris Saint-Germain, Vitinha na João Neves, kwa kusisitiza kuwa hakuna mpango wowote wa wawili hao kuondoka klabuni hapo kuelekea Real Madrid kama ilivyokuwa ikidaiwa katika siku za hivi karibuni.
Mendes amesema kuwa majina ya viungo hao wa kimataifa wa Ureno hayajawahi kujadiliwa katika mazungumzo yoyote ya usajili, akikanusha uvumi uliokuwa ukienea kuhusu mustakabali wao. “Vitinha na João hawakuwa chaguo kwa mtu yeyote. Hawauzwi na Paris Saint-Germain na wana furaha kubwa ndani ya klabu hiyo,” alisema Mendes.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Real Madrid imekuwa ikitajwa kuendelea kutafuta viungo wa kiwango cha juu kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake. Hata hivyo, Mendes amesisitiza kuwa PSG hawana nia ya kuachana na wachezaji hao kutokana na mchango wao mkubwa ndani ya timu.
“Wataendelea kubaki PSG na kuendelea kukusanya mataji,” aliongeza Mendes, akionyesha imani yake kuwa wawili hao bado wana nafasi kubwa katika mipango ya muda mrefu ya mabingwa hao wa Ufaransa.
Tamko hilo linaonekana kufunga mjadala uliokuwa ukiendelea kuhusu uwezekano wa Real Madrid kuwafuata nyota hao wa Ureno. Kwa sasa, Vitinha na João Neves wanatarajiwa kuendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha PSG kinacholenga kutetea mataji ya ndani na kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya Ulaya msimu ujao.


