Kama wewe ni mpenzi wa michezo na hupendi kubaki nyuma kwenye habari mpya, Meridian Sports App imekuja kukusogezea kila kinachoendelea kwenye ulimwengu wa michezo. Kupitia simu yako, unaweza kufuatilia habari mbalimbali kutoka Tanzania, Afrika na duniani bila kuzunguka huku na kule kutafuta taarifa.
App hiyo inapatikana kwa watumiaji wa Android kupitia Google Play Store, wakati wenye iPhone kupitia App Store. Baada ya kuipakua, shabiki anapata nafasi ya kufuatilia taarifa za michezo kwa urahisi, kuanzia habari za timu, wachezaji, mechi na matukio mengine yanayotikisa ulimwengu wa michezo.
Kwa upande wa soka, Meridian Sports App inakuletea habari kutoka kwenye ligi kubwa duniani kama EPL, LaLiga, Serie A, Ligue 1, Bundesliga, Saudi Pro League pamoja na Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Hii inamaanisha kama ni habari za usajili, matokeo, wachezaji au kinachoendelea kwenye timu yako, unaweza kuwa karibu na taarifa hizo kupitia app hiyo.
Sio soka tu, kwani app hiyo pia inakupa habari za mashindano makubwa kama UEFA Champions League, Europa League, Conference League, CAF Champions League na CAF Confederation Cup. Pia, mashabiki wanaweza kupata habari kuhusu maisha ya wachezaji nje ya uwanja pamoja na michezo mingine kama Basketball, Boxing, Tennis na Riadha.
Kwa kifupi, kama unataka habari motomoto za michezo zikutokee hapohapo, Meridian Sports App ni sehemu ya kuanzia. Pakua app hiyo kupitia Google Play Store au App Store, kisha endelea kufuatilia habari, matukio na stori zinazotikisa ulimwengu wa michezo muda wowote na popote ulipo.


