Merino asema anaishi ndoto baada ya kuipeleka Hispania nusu fainali

Kiungo wa Hispania, Mikel Merino, amesema anahisi kama anaishi ndoto baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi katika dakika ya 88 dhidi ya Ubelgiji na kuipeleka Hispania hatua ya nusu fainali ya michuano  ya Dunia 2026. Hilo ni bao la pili mfululizo la ushindi alilofunga katika hatua za mtoano, baada ya kufunga pia muda wa nyongeza dhidi ya Ureno.

Merino asema anaishi ndoto baada ya kuipeleka Hispania nusu fainaliMerino alisema hakuwahi kufikiria angeweza kuandika historia hiyo katika mechi mbili mfululizo. “Singeweza kuwaza jambo kama hili hata katika ndoto zangu za mbali. Nilidhani ingenichukua muda mrefu kurudia kufunga bao la ushindi dakika za mwisho, lakini nimefanikiwa kufanya hivyo tena katika mechi iliyofuata,” alisema nyota huyo wa Arsenal.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Bao la ushindi lilitokana na shuti la Pau Cubarsi ambalo lilimponyoka kipa wa akiba wa Ubelgiji, Senne Lammens, kabla ya Merino, ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika mbili tu zilizopita, kuuwahi mpira na kuutumbukiza wavuni. Merino alisema mafanikio hayo hayakuwa ya bahati bali yametokana na kujituma na kujiamini kila anapopewa nafasi ya kucheza. “Ninaingia uwanjani nikiwa na ari kubwa na imani kwamba ninaweza kusaidia timu popote ninapohitajika. Ndivyo nilivyofanya tena,” alieleza.

Merino asema anaishi ndoto baada ya kuipeleka Hispania nusu fainaliAkizungumzia safari ya Hispania kwenye michuano ya Dunia, Merino alisema imekuwa ngumu zaidi kuliko ilivyokuwa katika ushindi wao wa Euro miaka miwili iliyopita. “Tumepambana sana leo. Labda safari hii haijawa ya kuvutia kama ilivyokuwa Euro, lakini muhimu ni kwamba tumeendelea mbele,” alisema.

Merino asema anaishi ndoto baada ya kuipeleka Hispania nusu fainaliSasa Hispania itakutana na Ufaransa katika hatua ya nusu fainali, mchezo ambao Merino anaamini utakuwa wa kiwango cha juu. “Itakuwa vita ya kweli kwa sababu ndivyo ilivyo kwenye nusu fainali. Ufaransa ni moja ya timu bora, lakini nasi tuna njaa ya ushindi. Ni mechi ya kiwango cha juu kabisa na tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunafika fainali,” alisema Merino.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.