Mtaalamu wa zamani wa mpira wa miguu wa Uingereza, meneja na mchambuzi wa televisheni wa michezo wa Sky sports Paul Merson amesema kuwa kumpa unahodha kiungo mshambuliaji wa Arsenal Martin Odegaard inaweza kuwa ni mafanikio kutoka kwa Mikel Arteta.

Odegaard walimnunua  kwa dau la Euro35M kutoka Real Madrid na kwasasa anaonyesha kiwango kikubwa katika vinara hao wa ligi mpaka sasa.Kiwango chake kimekuwa cha kuvutia sana baada ya kufunga mabao mawili kwenye mechi dhidi ya FC Bournemouth, na bao moja kwenye mechi dhidi ya Fulham.

Merson: Odegaard Kuwa Nahodha

Vilevile ameongezea kwa kusema ni mwanzo mzuri wa Odegaard kama nahodha kwani  huchukua muda kuzoea mazingira ya klabu moja ukiwa umehamia kutoka Real Madrid, lakini pia Madrid ni klabu kubwa na ana uhakika kuwa angetaka kurudi Real baada ya mkopo wake wa kuwa Arsenal kumalizika. Lakini Arteta amemfanya abaki na sasa anaonyesha yeye ni mchezaji wa aina gani.

Merson: Odegaard Kuwa Nahodha

Mpaka sasa Arsenal ndio timu pekee ilishinda mechi zake zote nne toka ligi iliporejea na akiwa na alama 12 kwa mechi alizocheza huku pia usajili wao waliofanya msimu huu wa kumsajili Gabriel Jesus kuonekana kuzaa matunda na wanashiriki michuano ya Europa barani Ulaya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa