Nyota wa klabu ya Paris Saint German Lionel Messi amesema kwasasa ana furaha klabuni hapo tofauti na mwaka uliopita ambao ndom ulikua mwaka wake wa kwanza ndasnin ya timu hiyo.

Mchezaji huyo akiongea baada ya mchezo wa timu yake ya taifa ya Argentina uliokua ukikipiga na Hondurus na kushinda kwa jumla ya mabao matatu kwa bila staa huyo ndipo alipozungumza.

“Najiskia vizuri kwasasa,Nafikiri imekua tofauti na mwaka ulioisha”Nilijua itakuja kua hivi”alisema Messi.

messi“Najiskia kupata utulivu klabuni,vyumba vya kubadilishia nguo,wachezaji wenzangu,mchezo wenyewe, pia nimeanza kujifurahia tena”.

Messi alipitia kipindi kigumu katika klabu wakati amejiunga kutokea klabu ya Fc Barcelona kuanzia kuanzia mazingira mpaka ubora ambao alikua anaounesha uwanjani.

Tangu kuanza kwa msimu mchezajji huyo bora wa dunia mara saba amekua na kiwango bora sana ni kama amezaliwa tena upya kutokana na kiwango anachokionesha kuanzia kwenye klabu hiyo mpaka timu ya taifa.

Katika mchezo uliopigwa jana kati ya Argentina na Hondurus ambapo staa huyo alifunga bao moja kumfanya kuendelea kukaa kileleni kwa wafungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa hilo baada ya kufikisha magoli 88.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa