COLLINS Opare ambaye ni raia wa Ghana kwa mara ya kwanza ameipa pointi tatu Dodoma Jiji mbele ya Geita Gold kwenye mchezo wa ligi kuu.
Dodoma Jiji kwa mara ya kwanza imeibuka na ushindi tangu msimu huu wa 2022/23 uanze chini ya Kocha Mkuu, Masoud Djuma.
Leo kwenye Uwanja wa Liti Singida, Dodoma imefanikiwa kuibuka na ushindi huo ambapo bao pekee la mchezo huo likifungwa na Collins Opare Dakika ya 30.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji, Mohamed Muya amesema: “Tunamshukuru Mungu tumepata matokeo mazuri na hii ni baada ya kufanya marekebisho kwenye maeneo yaliyokuwa na mapungufu ikiwemo eneo la ulinzi pamoja na ushambuliaji.”