Kwanza ufanisi wa kujipanga wa Simba ambayo Mugalu ndio anaitumikia. Simba walikuwa wanashambuliwa lakini walipoiba mpira katikati ya kiwanja walipiga pasi mbili tu kisha mpira ukafuatwa kambani.
Mugalu
Mugalu

Inadaiwa kwamba unapokuwa unashambuliwa, umbo lako linakuwa limeharibika. Si rahisi kupika goli mara moja unapotoka kushambuliwa.

Lakini watazame Simba, Miquissone aliuzima mpira katikati, wakati huo Bernad Morrison alishajitega njiani pembeni, halafu Mugalu alijificha nyuma ya mabeki wa kati. Lile bao lilikuja kwasababu ya uelewa mzuri wa kujipanga.

Pili, itazame pasi ya Bernad Morrison. Beki mmoja alikuwa anaelekea kumzuia Morrison ili kuiba muda wa wenzake kufika, mwingine alikuwa anaenda kuziba nafasi ya Mugalu.

Ilihitajika Pasi ya nguvu sana ya kupita katikati ya kipa na wale mabeki halafu iishie kwenye njia ya Mugalu, kosa dogo tu la upigaji pasi kila kitu kingeharibika, lakini tazama Morrison alivofanya kwa urahisi Super.

Mugalu

Mwisho kabisa mtazame Mugalu. Wakati Morrison anakimbia pembeni, na mabeki wanaelekea katika nafasi zao, mmoja wao ambayo ni Juma Nyosso akiwa anamfanyia marking, alihitaji akili sana kufunga, kwanini??

Alitakiwa akimbie nyuma ya Juma Nyosso kwasababu mbili, kwanza kukwepa kuwa offside. Pili, ili akutane na pasi ya Morrison mbele yake. Angewahi kidogo au kuchelewa angepishana na mpira. Ilihitajika Timing ya kiwango cha juu sana kama aliyokuwa nayo pale.

Bao la kawaida sana machoni lakini lililopikwa kwa ustadi wa hali ya juu sana.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa