Mgunda: Bado Kuna Mapungufu

LICHA ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema bado kuna mapungufu kwenye kikosi chake.

Mgunda tangu achukue kijiti cha kukinoa kikosi hicho amefanikiwa kuwa na mwenendo mzuri kwani katika mechi zote za kimashindano hajapoteza mchezo wowote.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mgunda alisema: “Mchezo umemalizika salama, nawashukuru vijana wangu kwa kutekeleza yale ambayo tumekuwa tukielekezana.

“Tumepata ushindi ni jambo jema kwetu lakini kuna mapungufu nimeyaona kwenye kikosi, tunaenda kuyafanyia kazi ili yasijirudie kwenye mchezo ujao na kuendelea kuwa bora zaidi ya leo.”

Baada ya mchezo huo, Simba inatarajia kusafiri kuelekea nchini Angola kumenyana na De Agosto kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano ya Klabu bingwa barani Afrika.

Acha ujumbe