Mgunda:KAMA ulidhani Simba SC wameridhika na ushindi walioupata kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Nyasa Big Bullet basi sio hivyo bali hawajamaliza.

Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa wamejifunza kulingana na makosa yaliyofanyika msimu uliopita hivyo mechi haijaisha mpaka filimbi ya mwisho.

Mgunda: Haijaisha Mpaka Filimbi ya Mwisho

“Tunajua kwamba klabu imetupa malengo yake hivyo kwetu kwa pamoja tunatakiwa kufika pale, tupo tayari kufikia malengo ya klabu.

“Kwa ujumla ni kwamba mimi pamoja na benchi la ufundi maandalizi ya mchezo wa kesho yamekamilika. Tuwaombee vijana walale salama na kesho waamke salama ili kukamilisha wajibu wao.

Mgunda: Haijaisha Mpaka Filimbi ya Mwisho
Juma Mgunda, Simba

“Binadamu anajifunza kwa makosa mechi inaisha mpaka filimbi ya mwisho, mechi ya Malawi ilikuwa kipindi cha kwanza wachezaji wanatambua hilo na wapo tayari kupambana.

“Mafanikio yote mazuri sio ya mtu mmoja, muunganiko nilioukuta, umoja uliopo, ari iliyopo kwa wachezaji na ahadi waliyonipa siku ya kwanza, wachezaji wanajua jukumu lao naamini watafanya vizuri hivyo tumejiandaa kiufundi kwenda kupambana.”

Mgunda: Haijaisha Mpaka Filimbi ya Mwisho

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa