Minziro Atoa Matumaini Mapya Fountain Gage fc

Kocha Mkuu wa Fountain Gate FC, Fred Felix Minziro, amesema licha ya mwanzo wa msimu kutokuwa kama walivyotarajia, benchi la ufundi limebaini maeneo ambayo timu ilifanya vibaya na sasa linafanyia kazi mapungufu hayo. Minziro amesema tathmini yao haiangalii matokeo pekee, bali pia namna timu inavyocheza na makosa yanayojitokeza ndani ya mchezo.

Minziro Atoa Matumaini Mapya Fountain Gage fcMinziro amesema mazoezi yamekuwa sehemu muhimu ya kurekebisha changamoto hizo, huku wachezaji wakisisitizwa kuongeza umakini, nidhamu na kufuata maelekezo wanapokuwa uwanjani. “Tunajua tulipokosea. Tumeyaona maeneo ambayo hatukuwa vizuri na tunafanyia kazi mazoezini,” amesema Minziro.

Kocha huyo amesema baadhi ya changamoto zinatokana na kushindwa kutekeleza mipango iliyowekwa kabla ya mchezo, hivyo benchi la ufundi linaendelea kuwasaidia wachezaji kuelewa majukumu yao na kufanya maamuzi sahihi katika nyakati tofauti za mchezo. Ameongeza kuwa mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja, bali yanahitaji mazoezi ya kila siku na uelewano zaidi ndani ya kikosi.

Minziro Atoa Matumaini Mapya Fountain Gage fcKatika eneo la ushambuliaji, Minziro amesema Fountain Gate inahitaji kuwa makini zaidi kutumia nafasi inazotengeneza, wakati ulinzi nao ukiendelea kufanyiwa kazi ili kupunguza makosa yanayoweza kuigharimu timu. “Tunataka kuona timu inakuwa bora kutoka mchezo mmoja kwenda mwingine. Huwezi kurekebisha kila kitu kwa siku moja, lakini kama tunafanya kazi kwa bidii kwenye mazoezi, tunaamini mambo yatabadilika,” amesema.

Minziro Atoa Matumaini Mapya Fountain Gage fcMinziro amesema bado anaamini Fountain Gate FC ina kikosi chenye uwezo wa kufanya vizuri na amewataka wachezaji kuendelea kuamini mchakato huo. Kocha huyo amesema lengo ni kuona kila mchezo unaofuata ukionyesha maboresho, kuanzia umiliki wa mpira, ulinzi, ushambuliaji hadi matumizi ya nafasi, huku akisisitiza kuwa kazi kubwa iliyopo sasa ni kuhakikisha kile kinachofundishwa mazoezini kinaonekana uwanjani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.