Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera akiambatana na Viongozi wengine wa Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Mbarali wametembelea kambi ya timu ya Ihefu kwa ajili ya kuongeza morali.

Ikumbukwe Ihefu tangu kuanza kwa msimu huu haijafanikiwa kupata ushindi katika mchezo wowote huku ikitarajia kumenyana na KMC kwenye mchezo ujao wa ligi.

ihefu, Mkuu wa Mkoa Aongeza Mzuka Ihefu, Meridianbet

Akizungumza nao, Homera amesema: “Niwapongeze mmesajili vizuri, na tunawaomba wachezaji mpambane kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunapata ushindi kwenye mchezo ujao dhidi ya KMC.”

Kwa upande wa Nahodha wa kikosi cha Ihefu, Joseph Mahundi amesema: “Tunakushukuru sana kiongozi kwa kuja kutupa hamasa na sisi tunaahidi kwenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo ujao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa