Modric kiungo fundi wa klabu ya Real Madrid amefunguka kua anaamini timu hiyo itafanya vizuri kwenye eneo la katikati licha kiungo Carlos Casemiro kuondoka klabuni hapo.

Kiungo huyo aliekua anatengeneza utatu mtakatifu katika eneo la kiungo la Real Madrid akiwa pamoja na Modric,na Toni Kroos wakipata mafanikio makubwa katika wakati wao kabla ya kiungo huyo wa kibrazil kutimkia katika klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza.

modricKatika mahojiano yake aliyoyafanya Modric amesema ana matumaini makubwa ya Real kufanya vizuri zaidi kwenye eneo la katikati akisifu machaguo yaliyopo kwenye kikosi hicho eneo la katikati ambapo kunajengwa na wachezaji kama Luca modric,Toni kroos,Fede valverde,Eduardo camavinga,Arellien tchouameni, pamoja na Dani ceballos.

Modric anaeleza sifa za wachezaji wa eneo hilo “akisema mchezaji kama Tchouameni amezoea kwa haraka,huku Camavinga akiwa na mwaka wa pili klabuni lakini alikua na wakati mzuri sana katika mwaka wa kwanza,huku Valverde akiwa anafanya vizuri kwenye nafasi yake, kwa Kroos yeye amecheza hapa kwa muda mrefu,na Dani ceballos amekua akiisaidia sana timu alisema Luca”

Kiungo huyo raia wa Croatia anaamini wameanza mwaka vizuri na wataendelea vizuri kama walivyoanza kwakua wana timu imara na kuondoka kwa Casemiro sio changamoto kubwa sana kwakua wana wachezaji wengi kwenye eneo hilo na wenye ubora.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa