Mtendaji Mkuu wa AS Monaco, Thiago Scuro, amekiri kuwa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba, hajafikia matarajio yaliyowekwa tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu uliopita. Pogba anaweza kuondoka Monaco baada ya mwaka mmoja pekee licha ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Pogba alijiunga na Monaco baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa kutokana na tuhuma za matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku, lakini alishindwa kuonyesha kiwango chake cha zamani kutokana na changamoto za kiafya na utimamu wa mwili. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 amecheza mechi sita pekee katika mashindano yote tangu kuwasili kwake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Scuro alisema klabu bado inamheshimu Pogba kama mchezaji na kama mtu, lakini alikubali kuwa mpango waliokuwa nao haukuenda kama walivyotarajia. “Ni suala gumu kwa sababu tuna heshima kubwa kwa Paul na kwa mtu ambaye yeye ni. Tangu alipowasili amekuwa na mtazamo mzuri,” alisema Scuro.
“Hata hivyo, ni kweli kwamba msimu uliopita mradi wetu haukwenda vizuri. Tulipoanza naye majira ya joto, matarajio yalikuwa tofauti kabisa na kile kilichotokea,” aliongeza kiongozi huyo wa Monaco. Scuro amesema klabu itaendelea kufuatilia maendeleo ya Pogba kimwili na kiufundi kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.
Monaco kwa sasa inalenga kupunguza gharama za mishahara, jambo linaloweza kuathiri nafasi ya Pogba kubaki katika kikosi hicho. Kocha mpya wa Monaco, Filipe Luís, amemtaja Pogba kama “mchezaji wa kipekee” na anatarajiwa kufanya mazungumzo naye siku zijazo kabla ya uamuzi wa mwisho kufikiwa.


