Morocco Yaishangaza Dunia

Timu ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kuitupa nje timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mikwaju ya penati katika mchezo uliopigwa katika dimba la Education City.

Katika mchezo uliokua mkali na wa kuvutia kuanzia dakika ya kwanza mpaka dakika 120 zinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake kutokana na ubora ambao ulioneshwa na timu zote kwenye namna ya kuweza kuzuia lango lango.moroccoTimu ya taifa ya Hispania muda mwingi wa mchezo walionekana kutawala mpira na kushambulia kwa kasi lakini timu ya taifa ya Morocco walionekana kua makini zaidi kwenye kuzuia na kushambulia kwa kushtukiza mashambulizi ya hatari japo hawakuweza kupata bao.

Simba wa Atlas kama wanavyojulikana wamefanikiwa kuushangaza ulimwengu baada ya kuwatupa nje mabingwa wa zamani wa kombe la dunia Hispania baada ya kucheza kwa ubora mkubwa na nidhamu ya hali ya katika kuzuia. Timu hiyo imeshangaza wengi kuanzia hatua ya makundi nbaada ya kuongoza kundi mbele ya vigogo kama Ubelgiji na Croatia.moroccoPongezi za kipekee katika mchezo huo zinaenda kwa golikipa wa Morocco Bono ambaye aliwazuia Hispania kupata bao kwenye dakika tisini za mchezo baada ya kuchomoa michomo mikali na hata ilipofika hatua za upigaji wa penati golikipa huyo alichomoa penati tatu.

Acha ujumbe