Jose Mourinho anakiri kwamba ana miaka michache zaidi tu kabla ya pazia kuangukia kazi yake ya ukocha.

Mourinho mwenye umri 59, ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi kwenye Soka la kisasa, akishinda mataji mengi ya ligi nchini Uingereza, Hispania, Italia na Ureno huku akinyakua Ligi ya Mabingwa mara mbili.

 

Mourinho Ataja Lini Atastaafu.

Miaka ya hivi karibuni amekuwa na matokeo duni kwa mtaalamu huyu, ambaye anajikuta akiifundisha AC Roma na akiwa na taji la Ligi ya Europa tu la kuonyesha kwa misimu yake mitano iliyopita dimbani.

Wengi wamehoji iwapo, miezi minne kabla ya siku yake ya kuzaliwa ambapo atatimiza miaka 60, Mourinho anapaswa kuacha kazi yake ya Ukocha.

Ingawa anakiri kustaafu sio mbali sana bali ni hivi karibuni, Kocha huyo mwenyewe amefichua kuwa bado kuna miaka michache kabla ya kutafakari.

 

Mourinho Ataja Lini Atastaafu.

“Miaka hii 22 imepita haraka, lakini nataka kuendelea,” Mourinho alisema katika hafla ya Quinas de Ouro mwaka 2022.

“Ninajisikia vizuri, ninahisi nguvu, nina ari, napenda kushinda, nachukia kushindwa, hakuna kilichobadilika.”

“Rangi ya nywele zangu, ndiyo, hata mikunjo, lakini nataka kuendelea.”

“Si kwa miaka 22 zaidi, kwani hakuna wakati, lakini kwa miaka michache zaidi.”

 

Mourinho Ataja Lini Atastaafu.

Klabu yake ya Roma inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi ya Serie A baada ya kushinda mechi nne kati ya saba za kwanza msimu huu, nafasi ambayo walimaliza mwaka jana.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa