José Mourinho yuko hatua moja tu kutangazwa rasmi kama kocha mpya wa Real Madrid baada ya taarifa kueleza kuwa tayari amekubali kurejea Santiago Bernabéu kwa awamu ya pili ya kazi yake ya ukocha.

Kocha huyo Mreno anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja zaidi endapo atafanikiwa kutwaa ubingwa wa La Liga. Ripoti zinaeleza kuwa kila kitu kiko tayari kukamilika mara tu msimu utakapomalizika rasmi na Florentino Pérez kuthibitishwa kuendelea kuwa rais wa klabu.
Mourinho anakuja Madrid baada ya kumaliza msimu na Benfica bila kupoteza mchezo wa ligi, lakini bado wakamaliza nafasi ya tatu nyuma ya Porto na Sporting CP, hali iliyowakosesha nafasi ya Champions League msimu ujao.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Inaelezwa kuwa Real Madrid tayari wamekubaliana mshahara na wakala wake Jorge Mendes, huku Mourinho akiwa na kipengele maalum kwenye mkataba wake Benfica kinachomruhusu kuondoka kwa euro milioni tatu tu. Aidha, Sky Sports imeripoti kuwa ataondoka na makocha wanne kutoka Benfica kwenda nao Bernabéu.

Kwa mashabiki wa Madrid, kurejea kwa Mourinho kunafungua ukurasa mpya wenye kumbukumbu kali. Katika kipindi chake cha kwanza kuanzia 2010 hadi 2013, aliwafanya Madrid kuwa moja ya timu kali zaidi katika historia yao, akivunja rekodi nyingi za La Liga na kuifanya Madrid kuwa mpinzani mkubwa wa Barcelona ya Pep Guardiola.



