Kocha mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho amesema Frank Lampard alikuwa kwenye hofu baada ya kufanya usajili uliyotumia pesa nyingi kwenye msimu uliyomalizika.

Spurs ya Mourinho wanaongoza msimamo wa Premier League na wanajiandaa kutembelea viunga vya Stamford Bridge siku ya Jumapili kwaajili ya debi ya London.

Baada ya kuwasaini wachezaji kama Kai Havertz, Timo Werner, Ben Chilwell, Hakim Ziyech na Edouard Mendy Chelsea wapo nafasi ya tatu kwenye jedwali la Premier League.

Mourinho: Lampard Alishikwa na Kitete Baada ya Usajili.
Wachezaji waliyo sajiliwa na Chelsea msimu 2020-21.

Sajili zote za Chelsea kwa ujumla zinaripotiwa kufikia kiasi cha £222m katika uwekezaji kwa msimu wa pili wa Lampard tangu achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo aliyowahi kuichezea zamani.

Mourinho, ambaye aliwahi kuifundisha Chelsea kwa vipindi viwili tofauti na aliwahi kumfundisha Lampard alisema matumizi ya pesa pia huleta uoga.

“Unapo pendwa, unajua kwanini unapendwa,”aliwaambia maripota.

“Na unatakiwa ukubali hilo, na unatakiwa ushughulike na aina hiyo ya presha na kuwajibika. Nilikuwa katika klabu ambayo tunaweza kusema ubingwa upo ndani ya soko kwa sababu ya nguvu kubwa ya uwekezaji na nilikuwa nikishughulika na aina hiyo ya presha.

“Kwa hiyo sasa siyo mimi tena wa kushughulika na presha hiyo hiyo ni wengine watakao kuwa na presha hiyo. Hiyo siyo kwetu.

Lampard hakukaa kimya naye pia alisema kulikuwa hakuna shaka yoyote kila kocha alikuwa lazima awe kwenye kaouga flani hivi.

“Wote tuna presha zinazo elekeana, siyo mimi pekee na Jose aliwahi kuwa hapa kama Meneja kwa hiyo anaelewa vizuri sana ,” Lampard.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

19 MAONI

  1. Hapo ni jino kwa jino, mwalimu na mwanafunzi wanakutana na aendapo Chelsea itashinda itaonyesha kwamba anaelewa somo na safari bado ndefu. Kwangu Lampard bado ni mwanafunzi anayejifunza,itachukua muda mrefu kupata mafanikio

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa