Kocha wa Everton FC, David Moyes, amesema anatamani kusaidia kuinusuru klabu yake ya zamani ya West Ham United dhidi ya kushuka daraja kwa kuifunga Tottenham Hotspur katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England msimu huu.
Spurs wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa nafasi ya 17 kwa tofauti ya pointi mbili juu ya West Ham walio nafasi ya 18. Ili kuepuka kushuka daraja, West Ham wanahitaji ushindi dhidi ya Leeds United sambamba na Spurs kupoteza dhidi ya Everton.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Moyes alisema angefurahia kuona West Ham wakibaki katika ligi hiyo kutokana na historia yake ndani ya klabu hiyo ambapo aliinoa kwa vipindi viwili tofauti kati ya mwaka 2017 hadi 2024.
“Ningependa kuisaidia West Ham kubaki kwenye ligi kama nitaweza,” alisema Moyes ambaye aliwahi kuiongoza West Ham kutwaa taji la UEFA Europa Conference League mwaka 2023.
Hata hivyo, kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 alisisitiza kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha Everton wanamaliza msimu katika nafasi nzuri zaidi, huku nafasi ya kumaliza ndani ya 10 bora ikiwa bado ipo. “Muhimu zaidi ni Everton kupata nafasi nzuri kwenye msimamo kwa sababu itatupatia fedha zaidi kutokana na nafasi yetu ya ligi,” aliongeza Moyes.


