Mshambuliaji wa Australia, Mitch Duke, ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa baada ya kulitumikia taifa hilo kwa zaidi ya muongo mmoja. Duke mwenye umri wa miaka 35 anaondoka akiwa ameichezea timu ya taifa ya Australia (Socceroos) mara 50, akihitimisha safari iliyojaa mafanikio na kumbukumbu muhimu katika historia yake ya soka.
Katika kipindi chake cha kuitumikia Australia, Duke alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki michuano ya Dunia la mwaka 2022 nchini Qatar, ambapo alifunga bao la kichwa dhidi ya Tunisia lililoipa Australia ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya Dunia baada ya miaka 12. Bao hilo limeendelea kutajwa kuwa moja ya matukio makubwa katika historia ya timu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Aidha, mshambuliaji huyo alitoa mchango mkubwa katika safari ya Australia kufuzu mashindano ya Dunia 2026 kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Saudi Arabia kwenye mechi za kufuzu mwaka jana. Hata hivyo, hakujumuishwa kwenye kikosi cha mwisho kilichoshiriki fainali za michuano ya Dunia zilizofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Duke alihitimisha kwa kueleza kuwa kufunga bao katika michuano ya Dunia mwaka 2022 ndilo tukio kubwa zaidi katika maisha yake ya soka. “Nitathamini kila kumbukumbu niliyopata, lakini kufunga bao kwa Australia kwenye michuano ya Dunia 2022 ndiyo kilele cha maisha yangu ya soka. Imekuwa heshima kubwa zaidi maishani mwangu kuvaa jezi ya Socceroos na kuiwakilisha nchi yangu,” alisema mshambuliaji huyo.


