Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars Simon Msuva ameeleza kuwa amekuwa akizungumza mambo mengi na Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi n ahata kuhusu kesi yake wakati ipo FIFA na alikuwa akimshauri mambo mengi.

Msuva amesema Hersi kwake ni kama kaka na amekuwa akizungumza naye mara kwa mara na vitu tofautitofauti na siyo yeye hata baadhi ya viongozi na watu wengine wa Simba na Yanga wamekuwa wakimuulizia kuhusu habari zake.

MSUVA

Akizungumzia mahusiano yake na Hersi Msuva alisema: “Eng. Hersi nimeshakutana naye sana ni kaka ambaye tunaongea mambo mengi hata kwenye hii kesi alikuwa akinishauri vitu vingi sana. Siyo yeye hata watu wa Simba walikuwa wakinipigia simu na kutaka kujua naendeleaje.”

Msuva kwasasa ni mchezaji huru baada ya kushinda kesi yake ya madai dhidi ya mabingwa wa Afrika Wydad Casablanca na Fifa kuiamuru klabu hiyo kumlipa fidia ya zaidi ya billioni 1.6.

Ikiwemo malimbikizo ya mshahara wa nyota huyo na ada yake ya usajili aliposaini kujiunga na miamba hiyo ya Morocco.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa