Kiungo mshambuliaji wa timu ya Bayern Munich Thomas Muller amesema kuwa Bayern lazima wajiangalie ikiwa wanataka kutetea ubingwa wa Bundesliga baada ya kulazimishwa sare ya tatu mfululizo

 

Muller: Bayern Lazima Tujiangalie

Leo nina hasira kwa mara ya kwanza, aliiambia Sky Sport.”Nimejichukia. Ikiwa tunataka kushinda kila mchezo, na hilo ndilo lengo letu, basi tunapaswa kucheza hadi dakika ya mwisho kabis. “Ikiwa tutakaa juu ya jedwali, lazima tujiangalie alisema Muller.

Nagelsman alifanya mabadiliko sita nyuma ya ushindi wa katikati ya wiki dhidi ya Intermilan kwenye ligi ya Mabingwa, na mtihani mwingine unakuja siku ya Juamnne ambapo atakipiga dhidi ya FC Barcelona ambapo itakuwa ni mechi ya kisasi kwa Barca ambapo msimu uliopita vijana wa Camp Nou walipigwa nje ndani jumla ya mabao 6.

 

Muller: Bayern Lazima Tujiangalie

Kocha wa timu huyo ambae ana umri wa miaka 35 aliiongoza Bayern kutwaa taji la 10 mfululizo la Bundesliga msimu uliopita, lakini kikosi chake kimeshinda tatu pekee kati ya tisa zilizopita za ligi hadi msimu uliopita. Alipoulizwa kocha huyo kuwa na presha  alisema kuwa;

 “Sijui kama presha iliongezeka. Presha daima ni ya mtu binafsi na jhutoka nje . Tutaendelea kufanya kazi, kufanya mazoezi hadi Jumatatu, kumchambua mpinzani na kujaribu kupata mawazo mazuri kwa ajili ya mchezo wa Barcelona.

Muller: Bayern Lazima Tujiangalie

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa