BONDIA namba moja nchini, HASSAN MWAKINYO, amefungiwa kupigana, na bodi ya usimamizi wa ngumi nchini Uingereza (BBBC), kwa muda usiojulikana, ikiwa ni siku chache tangu apoteze dhidi ya LIAM SMITH wa Uingereza.
Kwanini amefungiwa?
(I). Kwa sababu za kiafya, baada ya chama cha ngumi cha nchi husika kumpima na kugundua ana shida ya kiafya.
(II). Kupoteza pambano kwa Knock Out au Technical Knock Out.
(III). Kupoteza pambano katika namna isiyo ya kawaida, n.k.
Kufungiwa katika nchi moja kunaweza kumsababisha bondia asicheze au acheze kwenye mataifa mengine, kivipi.
Iwapo chama cha nchi inayoandaa pambano kitauliza sababu ya kusimamishwa kwa bondia kwa chama kilichomsimamisha.
Iwapo sababu ya kusimamishwa kwa Mwakinyo ikawa ni ya jumla inaweza kumfanya bondia asicheze kwenye nchi nyingine, na kinyume chake.
Bado haijafahamika ipi sababu rasmi ya kusimamishwa kwa MWAKINYO, lakini kwa sababu tajwa hapo juu uwenda ni kwa sababu alipoteza pambano lake kwa TKO au kutokana na jinsi alivyopoteza pambano hilo.
Kwa habari na matukio ya kimichezo na ya uhakika tembelea Youtube channel yetu Meridian Sport