Gennaro Gattuso anatarajiwa kuondoka katika nafasi yake kama kocha mkuu wa Italy baada ya kushindwa kuipeleka timu hiyo kwenye FIFA World Cup 2026, na kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, kuna wagombea watatu wakuu wa kuchukua nafasi yake.

Gattuso na wachezaji wake walishindwa kufuzu baada ya kupoteza fainali ya mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Bosnia and Herzegovina Jumanne usiku.
Azzurri walicheza wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja na hatimaye kupoteza kwa mikwaju ya penalti ugenini mjini Zenica, jambo linalomaanisha kuwa sasa wameshindwa kufuzu kwa mashindano matatu mfululizo ya Kombe la Dunia.
Kwa hivyo, soka la Italia linaelekea kwenye mabadiliko makubwa, huku Gennaro Gattuso akitarajiwa kuondoka katika nafasi yake hivi karibuni, Gianluigi Buffon akitarajiwa kuachia nafasi yake ya mkuu wa ujumbe, na Gabriele Gravina kuondoka kwenye nafasi ya Rais wa FIGC.
Kulingana na ripoti kutoka Sky Sport Italia na vyanzo vingine, kuna wagombea watatu wa awali wa kumrithi Gattuso kama kocha mkuu.




