Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Julian Nagelsmann, amesema beki Antonio Rüdiger yuko tayari kupewa muda zaidi wa kucheza wakati timu hiyo itakapovaana na Ecuador katika mchezo wa mwisho wa Kundi E wa mashindano ya Dunia 2026. Ujerumani tayari imefuzu hatua ya mtoano, lakini inalenga kumaliza hatua ya makundi kwa ushindi wa tatu mfululizo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza kuelekea mchezo huo, Nagelsmann alieleza kuwa Rüdiger ameonyesha maendeleo makubwa ya kiafya baada ya kupona tatizo la goti lililomlazimu kufanyiwa upasuaji mwaka mmoja uliopita. “Goti lake halimsumbui kwa sasa, anajisikia vizuri sana na ninaamini alifanya kazi nzuri alipoingia kwenye mchezo uliopita. Tunatarajia ataendelea kufanya hivyo tena,” alisema Nagelsmann kupitia mkalimani.

Kocha huyo pia alibainisha kuwa hana mpango wa kufanya mabadiliko mengi katika kikosi chake licha ya timu hiyo kuwa tayari imefuzu hatua inayofuata. Ujerumani imeonyesha kiwango bora katika michuano ya mwaka huu baada ya kushindwa kuvuka hatua ya makundi katika matoleo mawili yaliyopita ya michuano ya Dunia.
Wakati huo huo, mshambuliaji Deniz Undav amesema hana tatizo kuendelea kuanzia benchi ikiwa hilo litasaidia mafanikio ya timu. Mchezaji huyo wa Stuttgart, aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ivory Coast, alisema: “Kama nisingeridhika kuanzia benchi, nisingekuwa hapa kwenye mkutano huu wa waandishi wa habari. Nitatoa mchango wangu iwe ninaanza kikosini au ninaingia baadaye. Jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha tunashinda mchezo.”


