Klabu ya Newcastle United imetangaza rasmi kumsajili winga wa kimataifa wa Ivory Coast, Bazoumana Touré, kutoka klabu ya Hoffenheim ya Ujerumani kwa mkataba wa muda mrefu. Ingawa klabu hizo hazijaweka wazi ada ya usajili, vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa dili hilo lina thamani ya pauni milioni 43.
Touré mwenye umri wa miaka 20 anajiunga na Newcastle baada ya winga Anthony Gordon kuondoka kuelekea Barcelona katika uhamisho unaoripotiwa kufikia euro milioni 80 pamoja na nyongeza mbalimbali. Touré anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Newcastle dirisha hili baada ya kipa wa Ufaransa, Ewen Jaouen, kuwasili wiki iliyopita.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Nyota huyo alisema kutua Newcastle ni hatua kubwa katika ndoto zake za kucheza soka la kiwango cha juu, akieleza furaha yake ya kujiunga na moja ya klabu kubwa nchini England.

Touré alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya taifa ya Ivory Coast mwezi Oktoba mwaka jana na aliwakilisha nchi yake kwenyemichuano ya Dunia 2026, akicheza mechi tatu kabla ya Ivory Coast kuondolewa katika hatua ya 32 bora baada ya kufungwa mabao 2-1 na Norway.


