Neymar Atangaza Kustaafu Timu ya Taifa Baada ya Kipigo Jana

Nyota wa Brazil, Neymar Jr, ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Brazil muda mfupi baada ya kuondolewa katika hatua ya 16 bora ya Taji la Dunia 2026 kwa kufungwa mabao 2-1 na Norway.

Neymar Atangaza Kustaafu Timu ya Taifa Baada ya Kipigo Jana

Neymar, mwenye miaka 34, alifunga bao pekee la Brazil kwa mkwaju wa penalti katika dakika za nyongeza lakini halikutosha kuizuia timu hiyo kuaga mashindano hayo huku Norway ikitinga robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo aliaanzia benchi kutokana na kusumbuliwa kwa majeraha ya hapa na pale hivyo kwenye mechi zote toka hatua ya makundi hajaanza kwenye kikosi cha kwanza.

Vijana hao wa Ancelotti licha ya kupata nafasi kipindi cha kwanza walishinda kuzitumia vyema na kuzifanya kuwa magoli lakini pia wlaiendelea kukosa nafasi za wazi kama ile ya Endrick na hivyo kuaga mashindano hayo.

Baada ya mchezo huo, Neymar alitangaza kuwa amefikia mwisho wa safari yake na timu ya taifa ya Brazil, akisema amefanya kila alichoweza kwa ajili ya nchi yake.

 

Neymar Atangaza Kustaafu Timu ya Taifa Baada ya Kipigo Jana

Neymar ameiwakilisha Brazil katika fainali nne za Taji la Dunia kuanzia mwaka 2014, lakini hakufanikiwa kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa dunia.

Anaondoka akiwa mfungaji bora wa muda wote wa Brazil, akiwa na mabao 80 katika mechi 130 alizoichezea timu hiyo ya taifa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.