Nyota wa Brazil, Neymar Jr, amerejea uwanjani kwa kishindo baada ya kufunga mabao mawili na kuiongoza Santos kutoka nyuma hadi sare ya mabao 2-2 dhidi ya Chapecoense katika mchezo wa Ligi Kuu ya Brazil uliochezwa Jumamosi.
Neymar, mwenye umri wa miaka 34, alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza tangu alipokaa nje kwa takribani miezi miwili na nusu kutokana na majeraha. Mabao yake yaliisaidia Santos kuokoa pointi moja muhimu, ingawa timu hiyo bado ipo kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa nafasi moja tu juu ya ukanda wa kushuka.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika siku za hivi karibuni, Neymar alikumbana na ukosoaji mkubwa baada ya kushiriki mashindano ya mchezo wa poker wakati wenzake walikuwa wakicheza mechi ya Copa Sudamericana nchini Venezuela. Kitendo hicho kilizua maswali kuhusu kujitolea kwake kwa timu.
Baada ya kufunga bao lake la kwanza, Neymar alionekana kujibu wakosoaji wake kwa kusherehekea kwa ishara ya kugawa karata, kabla ya kutumia bendera ya kona kuigiza mpigo wa mchezo wa gofu, ishara zilizotafsiriwa kama ujumbe wa kujibu ukosoaji aliokumbana nao.
“Ninaendelea kufanya ninachokipenda zaidi, ambacho ni kucheza mpira wa miguu. Majibu yangu bora siku zote yatakuwa ndani ya uwanja,” Neymar amesema, akionyesha kuwa anataka kiwango chake kiwe jibu kwa wakosoaji wake.
Neymar pia amefunga rasmi ukurasa wa maisha yake katika timu ya taifa ya Brazil baada ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa kufuatia Brazil kuondolewa na Norway katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Dunia, huku sasa akielekeza nguvu zake katika kuisaidia Santos kubaki Ligi Kuu ya Brazil.


