Beki wa klabu ya Borussia Dortmund na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Niklas Süle ametangaza kuwa atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu, akieleza kuwa uamuzi huo umetokana na sababu za kiafya na maisha yake binafsi.
Süle alithibitisha “Nataka kutangaza kwamba nitastaafu soka msimu huu wa kiangazi.” Mkataba wake na Borussia Dortmund unatarajiwa kumalizika Juni 30, 2026.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha, lakini amekuwa na historia ndefu ya kucheza Bundesliga ambapo amecheza mechi 299 na pia ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mara 49.
Akizungumzia sababu ya uamuzi wake, Süle alisema alifikia hatua hiyo baada ya kupata jeraha la goti alipokuwa akiichezea dhidi ya TSG Hoffenheim, klabu yake ya zamani. “Niliingia chumbani baada ya kipimo na nikalia kwa dakika 10,” alisema akieleza jinsi tukio hilo lilivyomgusa kihisia.
Aliendelea kusema kuwa hofu ya kupata jeraha jingine kubwa la goti ilichangia maamuzi yake. “Baada ya MRI na kupata majibu mazuri, ilikua asilimia 100 kwangu kwamba muda wangu umefika wa kuacha,” alifafanua.
Süle alijiunga na Borussia Dortmund akitokea Bayern Munich mwaka 2022, na tangu wakati huo amecheza mechi 109 na kufunga mabao matatu. Miongoni mwa kumbukumbu zake kubwa ni kufika fainali ya UEFA Champions League na kushiriki msimu uliokaribia kumpa ubingwa wa Bundesliga akiwa na Dortmund.


