Klabu ya Nottingham Forest ambayo imepanda ligi kuu ya nchini Uingereza inaendelea kujiimarisha katika dirisha hili kubwa la usajili baada ya kuendelea kufanya sajili mbalimbali za wachezaji ambapo beki wa kulia wa zamani wa Tottenham Spurs Serge Aurier anakaribia kujiunga na klabu hiyo akitokea Villareal ya nchini Hispania.
Nottingham Kumsajili Serge Aurier
Nottingham Forest kumsajili Aurier kutoka Villareal

Serge Aurier ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika mwezi uliopita  na sasa anatarajia kwenda kujiunga na Nottingham ambapo atasaini kandarasi ya miaka miwili katika uwanja wa City Ground kukitumikia kikosi hicho.

Nottingham Forest hawajaishia hapo tuu wapo kwenye mazungumzo ya  kumsajili beki wa kati wa Wolveshampton Wonderers Willy Bolly na kama watakamilisha usajili huo watakuwa na jumla ya wachezaji 20 ambao watakuwa wamesajili  kabla dirisha hili kufungwa Alhamisi hii.

Kutokana na klabu hiyo kumtaka beki huyo wa Wolves kocha wa timu hiyo Bruno Lage amesema kuwa Boly alikuwa kwenye list ya kikosi ambacho kilikuwa kinaenda kukabiliana na Newcastle United siku ya Jumapili lakini hakutokea.

Nottingham Kumsajili Aurier
Bruno Lage

“Nilimwambia ninahitaji mchezaji wa kiwango cha juu kama wewe kwenye benchi na baadaye akafanya uamuzi wake. Alikuwa kwenye orodha ya wachezaji na hakuja. Anataka kulazimisha kitu nafikiria”

Kwenye mechi nne ambazo Nottingham Forest wamekwishacheza wameshinda mechi moja, sare moja na wamepoteza mechi mbili huku wakiwa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa