Klabu ya Nottingham Forest imerejea katika ligi kuu ya Uingereza Premier League baada ya kuifunga Huddersfield bao 1-0 katika mchezo wa mtoano wa Championship siku ya Jumapili kwenye uwanja mashuhuri wa Wembley Stadium.

Nottingham Yarejea Premier League Baada ya Miaka 23

Hii inamaanisha Nottingham watashiriki msimu wa EPL 2022-23 kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 23 kuwa nje ya ligi hiyo maarufu ulimwenguni.

Bao la kujifunga la Levi Colwill kupitia pasi ya James Garner kwenye eneo la penati dakika ya 43 lilitosha kwa Forest kupanda kucheza EPL 2022-23.

Nottingham Yarejea Premier League Baada ya Miaka 23

Ushindi huo ulikamilisha msimu mzuri kwa Forest, ambao walikuwa mkiani mwa jedwali baada ya mechi nane wakati Steve Cooper alipochukua nafasi mwishoni mwa Septemba.

Ratiba ya msimu wa Ligi Kuu ya 2022/23 itatolewa Alhamisi, Juni 16. Ratiba ya EFL itakuwa Alhamisi, Juni 23.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa