Nuno Ataka VAR Kuwa na Uamuzi wa Haki na Uthabiti

Kocha wa West Ham United, Nuno Espirito Santo amesema mfumo wa VAR unahitaji kuwa na uthabiti mkubwa katika maamuzi yake baada ya timu yake kunyimwa bao muhimu dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliopita.

Nuno Ataka VAR Kuwa na Uamuzi wa Haki na UthabitiWest Ham walidhani wamepata sare ya mabao 1-1 baada ya Callum Wilson kufunga bao dakika za majeruhi, lakini bao hilo lilikataliwa baada ya Pablo kuonekana kumfanyia faulo kipa wa Arsenal, David Raya.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mbali na bao hilo kufutwa, Nuno alieleza kutoridhishwa na matukio mengine mawili ya mchezo huo ambapo West Ham waliamini walistahili kupewa penalti, jambo lililoifanya klabu hiyo kuwasilisha malalamiko rasmi kwa bodi ya waamuzi ya PGMOL.

Nuno Ataka VAR Kuwa na Uamuzi wa Haki na Uthabiti“Tulifanya malalamiko na nafikiri ilikuwa kawaida kufanya hivyo ili kupata majibu ya maswali yanayoleta mashaka mengi,” alisema Nuno.

Nuno Ataka VAR Kuwa na Uamuzi wa Haki na Uthabiti“Kinachohitajika kwenye uamuzi wa waamuzi na VAR ni uthabiti. Itasaidia mchezo, itasaidia Premier League na zaidi ya yote itawasaidia wachezaji kuelewa kuwa hakuna mashaka wala maumivu ya maamuzi yasiyoeleweka,” aliongeza.

Nuno Ataka VAR Kuwa na Uamuzi wa Haki na UthabitiWest Ham wanatarajiwa kusafiri kucheza dhidi ya Newcastle United wakihitaji ushindi ili kujinasua kutoka eneo la kushuka daraja, huku Nuno akisisitiza kuwa tofauti ya maamuzi katika matukio yanayofanana ndiyo chanzo kikubwa cha lawama dhidi ya VAR.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.