Nahodha wa Norway, Martin Ødegaard, amesema kukutana na mchezaji mwenzake wa Arsenal FC, Declan Rice, katika mchezo wa robo fainali wa michuano ya Dunia dhidi ya England utakuwa mtihani mkubwa kwa timu yake. Norway itakutana na England katika uwanja wa Miami Stadium siku ya Jumamosi huku wachezaji hao wakigeuka kutoka marafiki wa klabu kuwa wapinzani.
Ødegaard ambaye pia ni nahodha wa Arsenal, atakutana na wachezaji wenzake wa klabu akiwemo Rice, Bukayo Saka, Noni Madueke na Eberechi Eze. Hata hivyo, amesema mawasiliano yao yamekuwa machache kwa kuwa kila mmoja anaangalia jukumu la kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano makubwa zaidi duniani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Si sana kuhusu utani. Nimezungumza na baadhi yao kidogo wakati wa mashindano, lakini tunafahamu ubora wao. Nawajua vizuri sana,” alisema Ødegaard. “Ni wachezaji bora wa kiwango cha dunia na wanachezea moja ya timu bora za taifa kwa sasa, hivyo itakuwa changamoto kubwa kwetu.”
Nahodha huyo wa Norway alitoa sifa maalum kwa Rice, ambaye ndiye mhimili wa kiungo cha England, akisema uwezo wake wa kucheza maeneo mengi uwanjani unaweza kuwa tishio kubwa. “Declan ni mchezaji anayetoa kila kitu kwa ajili ya timu. Anapigania kila mpira, analeta nguvu na ana uwezo wa kuisukuma timu mbele,” alisema.
“Yanaweza kufanya mambo mengi uwanjani. Anaweza kulinda, kushambulia, kutumia nguvu zake na pia ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Ni mchezaji kamili na itakuwa mtihani mzuri kwetu sote,” aliongeza Ødegaard. Aidha, alisema Norway imepata kujiamini baada ya kuiondoa Brazil, mabingwa mara tano wa dunia, katika hatua ya 16 bora na sasa wanaamini wanaweza kuandika historia zaidi.
“Mechi dhidi ya Brazil ilikuwa sawa, tuliingia kama timu iliyodharauliwa lakini tukaonyesha kuwa chochote kinawezekana kwenye soka. Tunaamini uwezo wetu na tumeonyesha dunia kuwa sisi ni timu nzuri,” alisema Ødegaard. “Ingawa tena tunaingia kama watu wasiotarajiwa kushinda, tutaandaa vizuri mchezo na kuona kitakachotokea.”


