Klabu ya Chelsea imekubaliana na klabu ya Bayer Leverkusen inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kumtoa kwa mkopo winga Callum Hudson Odoi na anatarajiwa kufika leo Ujerumani kwaajili ya vipimo vya afya.

Makubaliano hayo yameafikiwa kwa pande zote mbili baada ya Odoi kuonekana hana namba ndani ya Chelsea toka msimu uliopita, lakini vilevile klabu hiyo inayoongozwa na Thomas Tuchel ina mawinga wengi ambao wana viwango ukilinganisha na Odoi.

Odoi atolewa kwa mkopo leverkusen

Winga hao ni kama vile kina Christian Pulisich, Kai Harvetz lakini pia na ujio wa Raheem Sterling ambae amesajiliwa dirisha hili kubwa la msimu umefanya kuwa na ufinyu wa nafasi kwake kwani tokea mechi za nusu msimu hajacheza na hata ligi ilipoanza hajaweza kupata nafasi.

Na sasa ataenda kujiunga na Bayer Leverkusen kwa mkopo ambayo kwa msimu huu itashiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kufanya vizuri msimu ulipota na kumaliza nafasi nne za juu huko Ujerumani. Timu hiyo inayoongozwa na kocha Gerardo Seoane  mpaka sasa katika msimamo wa Bundesliga ipo nafasi ya 13  ikiwa  imekwishacheza mechi nne ushindi mara moja na kupoteza mara tatu.

Odoi, Odoi Atolewa kwa Mkopo Leverkusen, Meridianbet

Callum Hudson Odoi anaenda kutafuta changamoto nyingine huko ili aweze kuongeza kitu katika timu hiyo lakini pia kama ataweza kufanya vizuri zaidi anaweza kuishawishi timu hiyo kumnunua au pia abaki katika timu yake ya zamani Chelsea.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa