BAADA ya kuanza vizuri kampeni ya kusaka taji la Ligi Kuu Bara msimu huu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold juzi Jumatano, Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Zoran Manojlovic ‘Maki’, amewasifu wachezaji wake kwa kiwango bora, huku akimvulia kofia kiungo Mghana, Augustine Okrah kwa kuweka wazi kiungo huyo atafunga sana msimu huu.

Augustine Okrah
Augustine Okrah

Okrah ambaye amesajiliwa na Simba kutokea kikosi cha Bechem ya Ghana, juzi Jumatano akiichezea Simba mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu alifanikiwa kuhusika kwenye mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 akifunga bao moja dakika ya 37, na kutengeneza penalti ya Chama dakika ya 85.

Kocha Maki alisema: “Nimefurahishwa sana na kiwango ambacho kimeonyeshwa na wachezaji wangu katika mchezo wetu dhidi ya Geita Gold, tulikuwa na wastani mzuri wa kufanya vizuri kutokana na nafasi za kufunga mabao ambazo tuliweza kutengeneza.

Augustine Okrah
Augustine 

“Unaweza kuona mchezaji kama Okrah anaingia na kuonyesha uwezo mkubwa, nadhani kuendana na kipaji alichonacho kadiri muda utakavyokuwa ukiendelea, ataimarika zaidi na kufunga mabao mengi.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa