FC Bayern Munich imeweka mguu mmoja katika hatua ya robo fainali ya UEFA Champions League baada ya kuichapa Atalanta BC mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliochezwa jijini Bergamo. Ushindi huo mzito umeifanya Bayern kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele huku ikiwa imeiendeleza rekodi mbaya ya Atalanta katika michezo ya mtoano ya mashindano hayo. Olise Aongoza Maangamizi Bayern Ikiizamisha Atalanta UCL.

Timu hiyo inayofundishwa na Vincent Kompany ilianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza mapema baada ya kona iliyopigwa kwa ustadi kumkuta Serge Gnabry aliyetoa pasi iliyoishia kwa Josip Stanišić kufunga kwa karibu na lango. Bayern iliendelea kutawala mchezo na kuongeza bao la pili katikati ya kipindi cha kwanza kupitia Michael Olise aliyepiga shuti kali kwa mguu wa kushoto lililojaa wavuni.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Michael Olise aliendelea kung’ara katika mchezo huo baada ya kutoa pasi ya mwisho iliyomwezesha Serge Gnabry kufunga bao la tatu na kuiweka Bayern mbele kwa mabao 3-0 kabla ya mapumziko. Licha ya Atalanta kujaribu kujipanga, Bayern ilionekana kuwa bora zaidi katika kila idara ya mchezo.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ileile ambapo Nicolas Jackson alifunga bao la nne kufuatia shambulizi la kushtukiza lililotokana na mpira wa adhabu wa Atalanta. Bayern iliendelea kutengeneza nafasi nyingi huku kipa wa Atalanta Marco Carnesecchi akifanya juhudi kadhaa kuzuia mabao zaidi.
Hata hivyo juhudi hizo hazikuzuia wimbi la mashambulizi ya Bayern, kwani Michael Olise alifunga tena bao la tano kabla ya Jamal Musiala kuongeza la sita kwa kumalizia pasi ya Nicolas Jackson. Bao hilo lilihakikisha Bayern inaondoka na ushindi mkubwa ugenini.

Licha ya Mario Pašalić kufunga bao la kufutia machozi kwa Atalanta BC mwishoni mwa mchezo, timu hiyo sasa inahitaji muujiza mkubwa kusonga mbele. Kwa upande wa FC Bayern Munich, ushindi huo unaiweka karibu sana na robo fainali ambapo inaweza kukutana na mshindi kati ya Real Madrid CF au Manchester City FC.

