Mwamuzi wa kimataifa kutoka Somalia, Omar Artan, ameeleza masikitiko yake baada ya kunyimwa viza ya kuingia Marekani, hali iliyomnyima nafasi ya kushiriki kuchezesha fainali za mashindano ya Dunia 2026. Tukio hilo limekatisha ndoto yake ya kuwa sehemu ya mashindano makubwa zaidi ya soka duniani.
Artan amesema kukosa fursa hiyo ni moja ya nyakati ngumu zaidi katika maisha yake ya uamuzi, akieleza kuwa michuano ya Dunia hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne na kila mwamuzi hutamani kupata nafasi ya kushiriki. “Ilikuwa ndoto yangu kuchezesha Kombe la Dunia. Kukosa nafasi hiyo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu ni jambo lililoniumiza sana,” alisema Artan.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya huzuni hiyo, mwamuzi huyo amewashukuru mashabiki, waamuzi wenzake na wadau wa soka kutoka mataifa mbalimbali kwa sapoti waliompa tangu taarifa hizo zilipoibuka. “Upendo na faraja niliyopokea kutoka kwa watu duniani kote vimenipa nguvu ya kuendelea. Nawashukuru wote waliosimama nami katika kipindi hiki kigumu,” aliongeza.
Artan amesema kuwa, ingawa hakuwepo uwanjani, bado anaendelea kufuatilia kwa karibu mechi za mashindano ya Dunia kupitia runinga na kufurahia kiwango kinachoonyeshwa na waamuzi wenzake. Ameeleza kuwa anajivunia mafanikio yao na anatamani kuona waamuzi kutoka Afrika wakiendelea kufanya vizuri katika jukwaa la dunia.
Akihitimisha, Artan amesema tukio hilo halitazima ndoto zake za kuendelea kuhudumu katika mchezo wa soka. “Safari yangu haijaishia hapa. Ninaamini bado kuna fursa nyingine mbele yangu, na nitaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuzifikia,” alisema kwa matumaini.


