KALI Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara ni mgumu kwa kuwa kila timu inahitaji pointi tatu.

Ongala, Kali Ongala alia na ugumu wa Ligi Kuu, Meridianbet

 

Ongala amekuwa kwenye mwendo bora na kikosi cha Azam FC ambapo mchezo wake wa kwanza aliwatungua Simba bao 1-0 Uwanja wa Mkapa na mtupiaji alikuwa ni Prince Dube.

 

Ongala

Ushindi mkubwa ambao ameupata akiwa kwenye benchi la ufundi ni ule wa Mtibwa Sugar 3-4 Azam FC kwenye mchezo wa kukata na shoka uliochezwa Uwanja wa Manungu.

Mchezo wake uliopita alishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 3-2 Coastal Union na mchezo huo wachezaji wa Coastal Union walionekana kuleta vurugu kwa mwamuzi pengine labda ni kutokana na maamuzi yake kwenye mchezo huo jambo ambalo linafuatiliwa na kamati kwa sasa.

Ongala amesema:”Kila mchezo ni mgumu na wapinzani wanafanya kazi kubwa kusaka matokeo, kikubwa ni kuona tunashinda na kupata pointi tatu,”.

Azam FC imekusanya pointi 32 baada ya kucheza mechi 14 kwenye msimamo ipo nafasi ya pili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa