Nyota chipukizi Nico O’Reilly alifunga mabao mawili kipindi cha pili na kuisaidia Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal katika fainali ya Kombe la Carabao (EFL Cup).
Arsenal walionekana kuanza mchezo kwa nguvu wakitengeneza nafasi kadhaa kupitia Kai Havertz na Bukayo Saka, lakini juhudi zao zilikwama baada ya kipa James Trafford kuokoa hatari tatu mfululizo na kuinyima mabao ya mapema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kadri mchezo ulivyoendelea, Manchester City walizidi kumiliki mpira na kutengeneza nafasi kupitia Antoine Semenyo na Erling Haaland, lakini safu ya ulinzi ya Arsenal iliendelea kuwa imara hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa presha kubwa kutoka kwa City, na hatimaye walipata bao la kuongoza dakika ya 60 baada ya krosi ya Rayan Cherki kumpita kipa Kepa Arrizabalaga na kumkuta O’Reilly aliyefunga kwa kichwa ndani ya eneo la hatari.
Dakika nne baadaye, O’Reilly aliongeza bao la pili kwa kichwa kingine safi kufuatia krosi ya Matheus Nunes, akiiweka City katika nafasi nzuri ya kushinda mchezo huo. Licha ya juhudi za Mikel Arteta kufanya mabadiliko, Arsenal walishindwa kurejea mchezoni.
Akizungumza baada ya ushindi huo, kocha wa City Pep Guardiola alisema “Tulionyesha ubora na subira hadi tukapata mabao yetu. Ni ushindi mkubwa kwa timu na mashabiki wetu.”
Kwa upande wake Arteta alisema “Tulianza vizuri lakini hatukutumia nafasi zetu. Makosa madogo yametuadhibu na kutugharimu taji.”

