Kamati ya Waamuzi wa Ligi Kuu nchini Hispania inadaiwa kuchukua hatua dhidi ya mwamuzi Ortiz Arias kufuatia kiwango chake cha uamuzi katika mchezo wa dabi ya Madrid kati ya Atletico Madrid na Real Madrid uliochezwa wikiendi iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanahabari Garchivovar, Ortiz Arias anatarajiwa kusimamishwa kuchezesha mechi kwa angalau raundi mbili zijazo za La Liga. Hatua hiyo inatajwa kuhusishwa na tathmini ya uamuzi wake katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa.
Ortiz Arias amekuwa mwamuzi wa La Liga tangu msimu wa 2021/22, lakini mchezo huo ulikuwa mara yake ya kwanza kuchezesha Real Madrid tangu aanze kazi katika ligi hiyo. Hilo lilifanya dabi hiyo kuwa moja ya mechi kubwa zaidi katika kipindi chake cha uamuzi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mchezo kati ya Atletico Madrid na Real Madrid pia ulikuwa mechi kubwa ya kwanza kabisa ya kiwango hicho kwa Ortiz Arias katika misimu yake yote sita akiwa mwamuzi wa La Liga.
Iwapo taarifa za kusimamishwa kwake zitatekelezwa, Ortiz Arias atakosa angalau raundi mbili zijazo za La Liga kabla ya kurejea kwenye orodha ya waamuzi watakaopangiwa michezo. Hatua hiyo inakuja wakati kamati husika ikiendelea kutathmini viwango vya waamuzi baada ya michezo mikubwa ya ligi.


