Ouahbi Akiri Morocco Ilizidiwa, Aipa Hongera Ufaransa kwa Ubora Wake

Kocha wa Morocco, Mohamed Ouahbi, amesema kikosi chake kilikuwa na ndoto ya kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Dunia 2026, lakini kimekubali ukweli kwamba kilizidiwa na Ufaransa iliyoshinda mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Alhamisi. Hata hivyo, amesema wachezaji wake wanapaswa kujivunia juhudi walizoonyesha licha ya kuaga mashindano.

Ouahbi Akiri Morocco Ilizidiwa, Aipa Hongera Ufaransa kwa Ubora WakeOuahbi alisema baada ya mchezo kuwa amewataka wachezaji wake waendelee kuwa na imani na kutoinamisha vichwa kwa sababu walitoa kila walichokuwa nacho uwanjani. “Niliwaambia wachezaji wangu waendelee kuinua vichwa vyao. Tulitoa kila kitu tulichokuwa nacho, lakini sasa tunapaswa kujitathmini kwa uaminifu ili tuweze kuendelea kupiga hatua,” alisema kocha huyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo alikiri kuwa Ufaransa ilitawala mchezo tangu mwanzo, hasa kwa umiliki wa mpira na mashambulizi kupitia pembeni pamoja na katikati ya uwanja. “Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu sana. Walikuwa bora wanapokuwa na mpira na walitupa matatizo mengi. Sisi tulipoupata mpira hatukuwa na mpito mzuri wa mashambulizi, tulikosa ubunifu na nguvu za kutosha. Lazima tukubali kuwa walikuwa timu bora zaidi leo,” alieleza.

Ouahbi Akiri Morocco Ilizidiwa, Aipa Hongera Ufaransa kwa Ubora WakeOuahbi amesema ingawa kuzungumza mara baada ya kipigo si jambo rahisi, kufika robo fainali ni hatua nzuri kwa Morocco, lakini bado kuna maeneo mengi yanayohitaji kuboreshwa. “Hatupaswi kuridhika kwa kujivunia tu tulichofanya. Tunahitaji kujikosoa, kujifunza na kufanya kazi zaidi ili tuwe timu yenye ushindani mkubwa zaidi siku zijazo,” alisema.

Ouahbi Akiri Morocco Ilizidiwa, Aipa Hongera Ufaransa kwa Ubora Wake Akikumbushia kuwa Morocco pia iliondolewa na Ufaransa katika michuano ya Dunia la mwaka 2022 nchini Qatar, Ouahbi alisema anaamini timu yake inaweza kurejea ikiwa na nguvu zaidi ifikapo michuano ya Dunia 2030 ambalo Morocco itakuwa mwenyeji mwenza pamoja na Hispania na Ureno. “Leo Ufaransa walikuwa bora, lakini tuna uwezo wa kuendelea kukua na pengine baada ya miaka minne tukawaondoa wao. Wana kila sifa ya kutwaa ubingwa, lakini binafsi natumaini Ubelgiji ndiyo itakayofuzu kukutana nao hatua inayofuata,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.