Kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Mohamed Ouahbi, amesema hawana muda wa kusherehekea sifa wanazopewa baada ya kufanya vizuri katika michuano ya dunia, akisisitiza kuwa tathmini ya safari yao itafanyika baada ya kumalizika kwa mashindano. Morocco inajiandaa kukutana na timu ya taifa yaUfaransa katika hatua ya robo fainali.
Mchezo huo utakuwa marudio ya nusu fainali ya mashindano haya mwaka 2022 ambapo Ufaransa iliivunja ndoto ya Morocco ya kufika fainali. Hata hivyo, safari hii Morocco imeingia kwenye mchezo huo ikiwa na kujiamini zaidi, huku ikiwa si tena timu ya kushtukiza bali moja ya mataifa yanayowania ubingwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tutafanya tathmini mwishoni mwa mashindano. Sitazungumza chochote sasa kwa sababu bado tunaweza kufanya zaidi,” alisema Ouahbi. “Hatutaki kusikiliza watu wanaosema tulichofanya hadi sasa ni jambo kubwa. Tunataka kwenda mbali zaidi.”
Ouahbi amekiri kuwa Ufaransa inaingia kama timu inayopendwa kushinda kutokana na historia yake na ubora wa kikosi chake, lakini amesema Morocco itaingia uwanjani kupambana kupata ushindi. “Ufaransa ni timu bora kwenye karatasi, lakini tutafanya kila kitu kesho kushinda na kufuzu hatua ya nusu fainali,” alisema kocha huyo.
Ufaransa, mabingwa wa dunia mwaka 2018 na waliomaliza nafasi ya pili mwaka 2022, walitinga robo fainali baada ya kuifunga Paraguay kwa bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti wa nahodha Kylian Mbappé. Mbappé tayari amefunga mabao saba kwenye mashindano haya, akiwa nyuma ya Lionel Messi mwenye mabao nane. Morocco nayo imeonyesha kiwango bora baada ya kuvuka hatua ya makundi na kuziondoa Netherlands pamoja na wenyeji wenza Canada, huku Ouahbi akisisitiza wanahitaji kucheza kwa nguvu zote bila kujali mafanikio ya awali. “Hatupaswi kufikiria tumeshafanya vizuri kufika hapa. Zawadi kubwa ni kushinda taji la Dunia,” alisema.


