Cole Palmer amekiri kuwa ilikuwa ajabu kukutana na klabu yake ya zamani ya Manchester City alipofunga penalti dakika za mwisho huko London Magharibi.

 

Palmer Afichua Hisia ya Ajabu Dhidi ya City Katika Ligi Kuu ya Uingereza

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alivutia kwa mara nyingine tena klabu yake mpya na akajiweka kwenye orodha ya wafungaji mabao kwa mara ya nne kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.


Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Palmer aliiacha klabu yake ya utotoni majira ya kiangazi na akafichua kuwa ilikuwa ni jambo la ajabu kukutana na wachezaji wenzake wa zamani katika jezi nyingine.

Palmer Afichua Hisia ya Ajabu Dhidi ya City Katika Ligi Kuu ya Uingereza
 

Alisema: “Ilikuwa ajabu sana, ni mara yangu ya kwanza kucheza dhidi ya City. Nina heshima kubwa kwa klabu niliyokaa kwa miaka 15 na inapendeza kukutana na marafiki. Hatukubahatika kupata ushindi. Nina mashabiki wengi wa City ninaowafahamu lakini ni mchezo.”

Kulikuwa na shinikizo kubwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya umri wa miaka 21 kabla ya mkwaju wake wa penalti lakini Palmer anakiri kuwa alikuwa na uhakika alipoongeza kasi.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Palmer Afichua Hisia ya Ajabu Dhidi ya City Katika Ligi Kuu ya Uingereza

Aliongeza kuwa ilikuwa ni kusubiri kwa muda mrefu lakini alijiamini na  alitulia na kuzingatia.

City walidhani wameshinda mechi hiyo wakati kombora la Rodri lilipomshinda Thiago Silva na kumpita kipa wa Chelsea Robert Sanchez zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya mpira kumalizika.

Mabao mawili ya Erling Haaland yaliwaweka wageni mbele mara mbili lakini Chelsea waliendelea kupambana kupitia mabao ya Silva, Raheem Sterling na Nicolas Jackson.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa