Baada ya kumtambulisha George Semwogerere kuwa kocha mkuu, Uongozi wa Pamba umesema kuwa una matarajio makubwa na Kocha huyo katika mashindano ya Championship ili kuweza kufikisha malengo ya kuweza kupandisha timu Ligi kuu.

Kocha huyu mwenye uraia wa Uganda anachukua mikoba ya Yusuph Chipo huku akiwa amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia Pamba msimu huu.

Pamba, Pamba Yamnasa Kocha wa Kimataifa, Meridianbet

Ofisa habari wa Pamba Fc Johnson James amesema kuwa: “Tunaimani ataweza kufikia malengo yetu kwenye mashindano ya Championship, na tutakuwa na Benchi letu la ufundi imara na lengo letu kubwa ni kupanda Ligi kuu.

Tumejipanga haswa na tumemtambulisha kwa kuwa tulikuwa hatuna kocha mkuu na atatuongezea thamani, na uzito ili kuhakikisha timu inafanya vizuri kwenye mashindano haya.

“Tunapozungumza ni kocha wa timu ya maboresho ya timu ya Taifa ya Uganda kwaiyo sio kocha mdogo ambaye pengine watu wanamdhania, tunaimani ni kocha mwenye uzoefu mkubwa atakuja kuisimamia timu yetu na amefundisha vilabu mbalimbali ikiwemo Rwanda Ethiopia na Somalia atakuja kuongeza kitu na uzoefu wake katika soka la Afrika.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa