Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Bouna Thiaw, amesema bado kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa licha ya kikosi chake kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Iraq katika mchezo wa michuano ya Dunia 2026. Ushindi huo umeifanya Senegal kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu hatua ya 32 bora kama moja ya timu nane bora zilizomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi.
Senegal ilionyesha kiwango cha juu katika Uwanja wa Toronto baada ya kuitawala Iraq, ambayo ilicheza sehemu kubwa ya mchezo ikiwa na wachezaji 10. Ushindi huo pia umeweka rekodi ya kuwa ushindi mkubwa zaidi kuwahi kupatikana na timu ya Afrika katika fainali za michuano ya Dunia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Licha ya kufunga mabao matano, bado kuna maboresho yanahitajika. Nawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyoifanya, lakini tunapaswa kuendelea kuimarika,” alisema Thiaw baada ya mchezo huo. Aliongeza kuwa sasa timu yake inasubiri matokeo ya mechi nyingine ili kujua kama itafuzu hatua ya mtoano.
Kocha huyo alisema Senegal imejikusanyia pointi tatu na kwa sasa matumaini yao yapo kwenye matokeo ya makundi mengine. “Sasa tunapaswa kusubiri. Tuna pointi tatu, bado kuna mechi nyingine zinazochezwa, hivyo tuna matumaini Senegal itafuzu,” alisema. Kwa sasa Senegal ipo nafasi ya tatu katika Kundi nyuma ya Ufaransa na Norway.
Thiaw pia aliwasifu viungo Pape Gueye, aliyefunga mabao mawili, pamoja na mshambuliaji Sadio Mané kwa mchango wao mkubwa ndani ya kikosi. “Pape Gueye ameonyesha ari kubwa, huku Sadio Mané akiendelea kuwa mfano wa moyo wa kupambana na kujitoa kwa timu. Mashabiki wetu wamekuwa nguvu kubwa kwetu, nasi tutaendelea kufanya kila tuwezalo kuwafurahisha,” alihitimisha kocha huyo.


