Leandro Paredes amefichua kuwa ‘hakuwa na uhusiano‘ na Kylian Mbappe wakati alipokuwa PSG, licha ya wawili hao kutumia chumba kimoja cha kubadilishia nguo kwa misimu mitatu.

 

Paredes:Mbappe Hajawahi Kuwa Rafiki Yangu.

Muargentina huyo aliondoka PSG msimu huu wa joto na kujiunga na Juventus kwa mkopo wa msimu mzima, ambao unaweza kudumu kwa paundi milioni 19.5 iwapo timu hiyo ya Italia itaamua kuanzisha kipengele cha kumnunua kwenye mkataba huo.

Tangu aondoke Parc des Princes, Paredes amefunguka kuhusu uhusiano wake na Mbappe, akisisitiza yeye sio mtu wa kuzungumza juu yake kutokana na kwamba hakuna uhusiano kati yao.

“Mimi sio mtu wa kuzungumza juu yake,” aliiambia ESPN Argentina wakati alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Mbappe. “Nilikuwa na uhusiano na wale ambao nilikuwa na uhusiano nao. Lakini wale ambao sikuwa na uhusiano nao, siwezi kukuambia kuwahusu.”

 

Paredes:Mbappe Hajawahi Kuwa Rafiki Yangu.

Hii si mara ya kwanza msimu huu kwa Mbappe kuwa na uhusiano mbaya na mmoja wa wachezaji wenzake, ambapo kauli ya Paredes inajiri siku chache baada ya Neymar kuhusishwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Mbappe, huku wawili hao wa PSG wakiripotiwa kutofautiana.

 

Paredes:Mbappe Hajawahi Kuwa Rafiki Yangu.

Wachezaji hao wawili wameonyesha dalili za uhusiano mbaya uwanjani tayari msimu huu huku washambuliaji hao walipotofautiana mwezi mmoja uliopita, kwa mkwaju wa penalti wakati wa ushindi wa 5-2 wa timu hiyo ya Ufaransa dhidi ya Montpellier.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa